English | Français | Español | 日本語 | Русский | 中文 | Ελληνική | العربية | български език | Deutsch | Bahasa Indonesia | بهاس ملايو | Português | Kiswahili | Türkçe | Galego | Norwegian | Italian | Latvian | Swedish | Slovak | Slovenian | Lithuanian | Finnish | Mongolian

MKATIBA WA KIMATAIFA KUHUSU MAZINGIRA CHANGIZI

Mazingira changizi kama yanavyoeleweka ni jumla ya maisha katika dunia na mchanganyiko wa mahusiano baina ya vitu vyote vyenye uhai. Ni tofauti ziliopo baina ya vitu vyote vinavyoishi na ujumuishi wake katika makao kwa ujumla. Mazingira changizi huwesesha uhusiano wa kiujumla baina ya watu, wanyama, mimea, wadudu na vitu vyote katika sayari yetu.

Vizazi vijavyo vitaathirika vibaya kutokana na huharibifu wa mazingira changizi. Tunachukua hatua hivi sasa kulingana na kifungu nambari 25, ajenda ya 21 ili kulinda na kudumisha mazingira changizi. Sisi vijana tuna maono ya kuhifadhi na kudumisha mazingira changizi ili kuchangia katika ukuzaji wa mazingira bora ulimwengu wa sasa na siku zijazo.

Sauti ya vijana yafaa kujumuishwa isikike katika kongamano kuhusu na mazingira changizi ili kuupata mchango wa vijana katika harakati za baadaye kuhusu mazingira. Vijana wana jukumuu muhimu la kuyalinda mazingira changizi kupitia shughuli mwajafa. Muunganiko wao katika ulimwengu mzima ili kueneza harakati za kimazingira ni muhimu. Hawa vijana wana nafasi kubwa ya kutetea mazingira changizi na uhusiano mwema wa kimataifa ni muhimu ili kuudumisha wema wa maisha katika sayari hii.

Hata hivyo, serikai mbali mbali zina jukumu muhimu la kuhakikisha utunzi na udumishaji wa mazingira changizi. Wasiojali sheria zinazolinda mazingira changizi wafaa kuchukuliwa hatua kabambe kulingana na shughuli zao kinyume na matarajio kwa kuwaunga vijana, mazingira changiri na/au ubora wa maisha ya baadaye, serikali zinalazimika:

  • Kutambua mchango wa vijana katika kuhifadhi mazingira changizi.
  • Kutoa pesa za kulipa mafunzo kuhusu umuhimu wa mazingira changizi.
  • Kuhusisha vijana katika harakati za kutoa maamuzi muhimu kama vile kuwawezesha kusafiri na kuhudhuria kongamano na kusambaza ujumbe kwa vijana wengine kupitia kwa mikondo mbali mbali ya kuwaunga pamoja.
  • Kuweka mikakati ya kuwahusisha vijana katika kutekeleza maazimio bora yanayoibuka katika kongomano mbali mbali.
  • Kujumuisha mikakati ya kimawasiliano na mahusiano ya kimazingira katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu matumizi ya ardhi.
  • Kuanzisha namna ya kukagua uhusiano wa maji na mazingira katika mataifa yote ulimwenguni.
  • Kutoa wakati mwafaka wa kutamatisha shughuli za kuharibu mazingira changizi.
  • Kudumisha sheria na hatua nyingine za kuhifadhi mazingira changizi.
  • Kuanzisha na kujumuisha harakati za kuchangia hatua za maendeleo katika hali zote.
  • Kuhusisha miji, muiinamo au muinuko wa ardhi, sehemu za aktika katika mikango maalumu.

KUJITOLEA KWETU

Ili kufanikiwa katika maono tuliyonayo sisi ambao tumeyatia sahihi makala haya tunajitolea kutumia maarifa ujuzi na vifaa vyote tulivyonavyo ili kulinda na kuboresha mazingira changizi. Tumejitolea kikagua ufanisi wetu na kujumuisha bidii zetu ili kuwasilisha matokeo yake kila mwisho wa mwaka.

© Biodiversity Matters. All Rights Reserved. Lab5 Web Design & Development